Saturday, February 15, 2014

Mrisho Ngassa (kushoto) amefunga mabao matatu leo katika ushindi wa 5-2 wa Yanga dhidi wenyeji Komorozine mjini Moroni katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika. Mabao mengine ya Yanga yamefungwa nna Hamisi Kiiza kulia na Simon Msuva na sasa timu hiyo ya Dar es Salaam inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 12-2 baada ya awali kushinda 7-0, Ngassa akifunga hat trick pia na itamenyana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katika Raundi ya Kwanza mwezi ujao.


Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment