Sunday, February 9, 2014

SIMBA SC imelala bao 1-0 jioni ya leo mbele ya Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.Kwa mara nyingine leo kipa Ivo Mapunda amefungwa bao rahisi, baada ya kumtemea mpira mshambuliaji Fully Maganga dakika ya 29 kufuatia mpira wa adhabu.Wachezaji wa Simba SC walipambana sana kujaribu kusawazisha bao hilo tangu hapo, lakini Mgambo Shooting leo walisimama imara kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.Kwa matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 17, wakati Mgambo inatimiza pointi 12 na inaendelea kushika mkia.Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk57, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Awadh Juma/Uhuru Suleiman dk62, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe na Ali Badru/Haroun Chanongo dk46.Mgambo Shooting; Saleh Tendega, Bashir Chanache, Salim Kipaga, Bakari Mtama, Novaty Lufunga, Mohamed Samatta, Peter Mwalyanzi, Bolly Ajali, Fully Maganga Malima Busungu.


Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment