mmoja Raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kufuatia ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Komorozine ya Comoro jioni hii katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Ligi ya Mabingwa Afrika.Washambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa alifunga mabao matatu, Mrundi Didier Kavumbangu mawili, Mganda Hamisi Kiiza moja na lingine beki Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’.Kwa ushindi huo, Yanga sasa inahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 6-0 katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo ugenini ili kusonga mbele, ambako itakutana na Al Ahly ya Misri.Wauaji; Mrisho Ngassa kushoto akiwapungia mikono mashabiki baada ya kukamilisha hat trick katika ushindi wa 7-0 wa Yanga dhidi ya Komorozine jioni hii Uwanja wa Taifa. Wengine kulia kwake ni SImon Msuva na Didier Kavumbangu aliyefunga mabao mawiliKatika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hassan Mohamed Hagi, aliyesaidiwa na Hamza Hagi Abdi na Bashir Abdi Suleiman wote kutoka Somalia, hadi mapumziko tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0.Mabao hayo yalifungwa na Ngassa dakika ya 14 na Cannavaro dakika ya 20, wote wakitikisa nyavu kwa kichwa baada ya mipira kutoka pembeni.Ngassa alifunga akimalizia krosi maridadi ya Simon Msuva kutoka wingi ya kulia, wakati Cannavaro aliunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na David Luhende kutoka wingi ya kulia, kufuatia Mbuyu Twite kuchezewa rafu.Mahambuliaji Mganda Hamisi Friday Kiiza aliikosesha Yanga SC mabao zaidi ya manne kipindi cha kwanza kwa kushindwa kuepuka mitego ya kuotea aliyokuwa akiwekewa na mabeki wa Komorozine.Mrisho Ngassa alikuwa mwiba leoYanga ilitawala mchezo kipindi chote cha kwanza na kufanya mashambulizi mengi, lakini pamoja na kupata mabao mawili walitengeneza nafasi zaidi ya nane walizoshindwa kuzitumia. Kipindi cha pili, Yanga ilianza na mabadiliko, ikimpumzisha David Luhende na kumuingiza Kavumbangu ambaye alikwenda kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji hadi mabao matano zaidi yakapatikana.Kavumbangu mwenyewe alianza dakika ya 57 akimalizia pasi ya Haruna Niyonzima, akafuatia Kiiza dakika ya 59 akimalizia pasi ya Kavumbangu, Ngassa mara mbili mfululizo dakika ya 64 na 68 na Kavumbangu akahitimisha karamu ya mabao dakika ya 80.Kikosi cha Yanga kilikuwa; Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Rajab Zahir dk76, Frank Domayo, Simon Msuva/Hassan Dilunga dk71, Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza, Mrisho Ngassa na David Luhende/Didier Kavumbangu dk46.Komorozine; Attoumani Farid, Ali Mohamed Mouhousoune, Nizar Amir, Abdou Moussoidi Kou, Ahamadi Houmadi Ali, Moidjie Ali, Mourthadhoi Fayssol, Attoumane Omar, Mohamed Erfeda/Imroina Ismael dk30, Mouyade Almansour Nafouondi na Ahmed Waladi Mouhamdi/Ghaidane Mahmoud dk80.
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment